Jeshi latoa makataa kwa raia B Faso

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kanali Issac Zida Kiongozi wa jeshi nchini Burkina Faso

Kiongozi wa jeshi nchini Burkina Faso ameyaagiza makundi ya wanaharakati kwamba yana hadi jumapili jioni kuwasilisha orodha ya wagombea wa serikali ya mpito.

Luteni kanali Isaac Zida alikubali mpango wa serikali ya mpito na makundi ya wanasiasa siku ya alhamisi lakini kufikia sasa hakuna kiongozi aliyetajwa.

Makundi hayo yamekubaliana kuwasilisha orodha ya wagombea kwa baraza la watu 23 ambalo litamchagua kiongozi atakeyaeongoza serikali hiyo ya mpito.

Kanali Zida alichukua mamlaka kutoka kwa rais Blaise Campaore ambaye aling'atuliwa mamlakani baada ya maandamano ya raia mnamo mwezi Octoba.

lakini maandamano hayo yalizuka tena na kupinga uongozi wa Jeshi baada ya kanali Zida kuiahirisha katiba ili kukabiliana na utovu wa nidhamu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Raia wa Burkina Faso wakati wa maandamano .

Hatahivyo baada ya jamii ya kimataifa kutishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo Uongozi wa raia ulirudishwa.

Siku ya Alhamisi, makubaliano ya kuweka bunge na kiongozi wa mda wa taifa hadi pale uchaguzi utakapofanyika mwaka ujao yaliafikiwa.

Katika taarifa yake siku ya jumamosi ,kanali Zida alisema kuwa makundi ya raia yana hadi saa nane siku ya jumapili kutoa orodha ya watakaoliongoza taifa hilo kwa mda.

Vilevile aliongezea kuwa amerudisha utawala wa raia kwa wenyewe.