Raia wa Marekani akatwa shingo na IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Peter Kassig mda mchache kabla ya kukatwa shingo na wapiganaji wa IS

Kanda moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonyesha mauaji ya mtu wa kutoa huduma za misaada raia wa Marekani Abdul Rahman Kassig ambaye alikuwa anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita

Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.

Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.

Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.

Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.

Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.