Je,wanaume huvutiwa na wasichana wadogo?

Image caption Wapenzi wawili.

Idadi kubwa ya wanaume huwapenda wasichana walio na umri wa miaka ya 20,hii ni kulingana na utafiti uliofanywa nchini Finland.

Katika utafiti huo wanaume 12,656 na wanawake walio kati ya umri wa 18 hadi 49 walihojiwa.

Washiriki waliulizwa kuhusu umri unaowavutia pamoja na umri wanawake ambao walifanya mapenzi nao katika kipindi cha miezi 12 iliopita.

Kulingana na watafiti majibu yaliambatana na jinsia ,huku wanawake wakionekana kuvutiwa sana na wanaume wa umri rika lao ama wale wenye umri mkubwa kiasi.

Wanawake walio na umri wa miaka 20 walipendelea wanaume walio wakubwa wao kwa miaka 4.

Kwa upande mwengine wanaume walionekana kuwapenda wasichana walio katika umri wa miaka 20.