Wito kwa wakazi kujihami dhidi ya Boko:H

Image caption Emir Sanusi alikuwa gavana wa benki kuu ya Nigeria kabla ya kuteuliwa kama Emir Kaskazini mwa Nigeria

Emir wa Kaskazini mwa Nigeria, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kiisilmau wenye ushawishi mkubwa, ametoa wito kwa watu nchini humo kuchukua silaha na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa kiisilamu wa Boko Haram.

Emir huyo wa Kano, Muhammad Sanusi, amewaambia wakazi wasisubiri wanajeshi kuwalinda kutokana na magaidi.

Emir huyo ambaye alikuwa gavana wa benki kuu nchini humo kabla ya kuchukua wadhifa wake wa Emir, alitoa matamshi yake ya kutatanisha kwenye mkutano wa maombi.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kauli kama hii sio kawaida kutolewa kwani Emir huyo huyo hazungumzii sana maswala ya kisiasa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa wakiwahangaisha wananchi kwa miaka mitano sasa

Wapiganaji wa wa Boko Haram wanaendelea kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika sehemu kadhaa za Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, huku wakiteka miji na mijiji ambko wamekuwa wakiwataka wakazi kufuata sheria kali ya kiisilamu.

Sanusi alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali alipokuwa anafanya kazi yake ya benki, alisema kuwa watu hawapaswi kuogopa wanamgambo hao na kwamba wanapaswa kufanya wawezalo kujikinda kutokana na mashambulizi ya kundi hilo.

Mwandishi wa BBC anasema ingawa Emir huyo hakutaka kundi la Boko Haram, ilikuwa hatua ya kipekee kwa kiongozi kama huyo kuwataka watu kujihami dhidi ya Boko Haram.

Aanasema hii ni dalili tu ya mambo yalivyo nchini humo hasa katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.