Kanali ahukumiwa kunyongwa DRC

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waaandamaji wakipinga kuuawa kwa Kanal Ndala

Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.

Afisa anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni Mamadou Ndala mabaye kwa kiasi kikubwa aliamini katika vita dhidi ya kundi hilo la wapiganaji na ambaye aliuawa mwezi Januari mwaka huu.

Hata hivyo hukumu hiyo imetolewa kwa watuhumiwa nane ambapo kati ya hao mmoja ndiye Kanali Ndala aliyehukumiwa kifo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kanal Mamadou Ndala anayedaiwa kuuawa na njama za Kanal Birocho Nzanzu

Mahakama imebainisha kuwa Kanali Nzanzu amekuwa akitumiwa na waasi wa ADF kutoka Uganda kuandaa maujaji.