Akataa mumewe kuwa na rafiki wa kike

Image caption Msanii Mary J Blige na Mumewe Kendu.Mwanamuziki huyo na mumewe wamekubaliana kutokuwa na marafiki wa jinsia tofauti katika uhusiano wao.picha hii ni kwa niaba ya thegrio.com

Mwanamuziki Mary J Blige kutoka Marekani amekataa kumkubalia mumewe kuwa na rafiki wa kike.Je,kunani?

Msanii huyo wa siku nyingi anayefahamika zaidi kwa wimbo wake wa ''No More Drama'' ameolewa na meneja wake Isaac Kendu tangu mwaka 2003,na wamekubaliana kwamba hawatakuwa na marafiki wa jinsia tofauti kwa kuwa iwapo swala hilo litapuuzwa basi hakuna ndoa itakayodumu.

Katika mahojiano na gazeti la Stella,bi Mary alibaini kwamba ''marafiki wote wa kiume kwake na marafiki wote wa kike kwangu'',.

''Katika uhusiano wa ndoa hakuna cha yule ni rafiki yangu wa kike ama huyu ni rafiki yangu wa kiume'', hilo haliwezi kufanyika katika ndoa iwapo munataka ndoa yenu idumu.alisema mwanamuziki huyo.

Mary ni mama wa kambo wa watoto wa Kendu,ambao ni Jordan mwenye umri wa miaka 16,Briana mwenye umri wa miaka 18 na Nas mwenye umri wa miaka 15 kutoka kwa uhusiano mwengine.