Mechi za kimataifa za kirafiki zarindima

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alexis Sanchez wa Chile akishangilia goli

Baada ya uhondo wa michuano ya Kombe la Dunia ya 2014 iliyomalizika nchini Brazil mwezi Julai mwaka huu, miamba mbalimbali ya soka duniani imeendelea kumenyana katika michuano ya kirafiki ya kimataifa. Usiku wa kuamkia leo zimepigwa mechi kadhaa katika viwanja mbalimbali duniani.

Mjini Glassgow ndugu wawili Scotland na England walimenyana vilivyo huku England ikiishushia kipigo Scotland iliyokuwa nyumbani cha mabao matatu kwa moja.Nahodha wa England Wayne Rooney alipachika mabao mawili yanyomfanya kwa sasa amkaribie mfungaji bora wa muda wote wa England Sir Bobby Charton aliyefunga magoli 49, na sasa Rooney amefikisha 46.

Kwengineko Mjini Manchester Ureno ya Christiano Ronaldo imeifyatua Argentina ya Lionel Messi kwa bao moja bila, huku Brazil ikiwafunga Austria 2-1

Italia nao wakiibugiza Albania 1-0 na Romania wameitikisa Denmark 2-0. Nazo timu zenye upinzani wa jadi za Amerika Kusini Chile ilikubali kipigo cha bao 2-1 katika mchezo uliojaa ubabe na kutembezeana viatu.