Basi linalotumia kinyesi lazinduliwa

Image caption Basi linalotumia kinyesi na uchafu wa vyakula laanza kutumika nchini uingereza.

Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza.

Bio Bus,lenye viti 40 na ambalo linatoa huduma ya uchukuzi kati ya Bath na uwanja wa ndege wa Bristol ,linaweza kusafiri hadi maili 186 kwa kutumia tangi moja la gesi.

Gesi hiyo hupatikana kupitia kutibu maji taka na uchafu wa chakula usiofaa kwa matumizi ya binaadamu.

Uchafu unaopatikana katika abiria wa basi moja unaweza kutumiwa kutoa kawi ya kulisafarisha basi hilo kutoka Lands End hadi John O'Groats.

Basi hilo ambalo limepewa majina kadhaa ya kutungwa likiwemo lile la Basi la pili linapongezwa kama njia mojawapo ya kuchochea usafiri wa uma huku ukiimarisha ubora wa hewa jijini.

Gasi inayotumiwa kuliendesha gari hilo hutoka katika mradi wa maji taka wa Bristol ambao husimamiwa na GENeco ambyo ni kampuni tanzu ya Wassex Water.

Mohammed saddiq,meneja mkurugenzi wa kampuni ya GENeco ,anaamini chakula na maji taka yanaweza kutoa kawi ya Biomethane inayotoa gesi katika shirika la kitaiafa la gesi inayoweza kutoa gesi yenye uwezo wa kutumika katika nyumba 8,500 mbali na kuliendesha basi hilo la Bio.