Polisi wadhibiti ulinzi mjini Mombasa

Image caption Polisin wakidhibiti ulinzi Mombasa

Polisi waliojihami wanaendelea kushika doria katika barabara za mji wa Mombasa Pwani ya Kenya hata baada ya maombi ya Ijumaa

Hii ni baada ya vurugu kati ya polisi hao na vijana baada ya kufanya msako katika baadi ya msikiti mjini humo.

Misikiti ambayo ilifanyiwa msako ambako inaaminika mafunzo ya itikadi kali za kidini inafanyika, ni Swafaa na Minaa.

Polisi wanadai kuwa misikiti hii hutoa mafunzo ya itikadi kali ikilenga kuwaunga mkono wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia Al Shabaab.

Haki miliki ya picha afp getty
Image caption Polisi wanadai kuwa walinasa bendera hii na silaha zingine katika miskiti iliyofanyiwa msako

Vijana waliojaribu kuingia katika msikiti wa Swafaa kwa maombi ya usiku, walikabiliwa na maafisa wa usalama.

Kwa siku nne zilizopita, kumekuwa na hali ya taharuki katika mtaa wa Kisauni baada ya polisi kudfanya msako katika msikiti ya Swafaa na Minaa katika juhudi za kupambana na vijana wenye itikadi kali za kidini na magenge ya vijana wanaowahangaisha wakazi.

Polisi walinasa silaha na vifaa vya kulipua mabomu katika msako huo ulioanza Jumatatu huku zaidi ya watu 100 wakikamatwa kwa madai kuwa walikuwa wanapokea mafunzo ya itikadi kali za kidini huku wakijiandaa kujiunga na kundi la Al shabaab.

Polisi hawajawaruhusu watu kuingia katika misikiti hiyo, na polisi wanasema yeyote atakayekwenda kinyume ya hilo, atakabiliwa na tisho la kupigwa risasi.