Ebola:Fuo za bahari kufungwa Liberia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption ufuo wa bahari.

Polisi nchini Liberia wametangaza kuwa watafunga fuko zote za bahari kuanzia tarehe 29 mwezi Novemba hadi pale taifa hilo litakapo tangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umemalizwa..

Tarehe hiyo itakuwa ni siku ya taifa la Liberia ya kuadhimisha kuzaliwa kwa raisi aliyeiongoza Liberia kwa miaka mingi William Tubman.

Polisi wanasema kuwa yeyote atakayetumia fuo hizo za bahari atakuwa amekiuka amri hiyo na atachukuliwa hatua za kisheria.

Polisi pia wamepiga marufuku mikutano yote ya umma isipokuwa ya kisiasa.

Karibu watu 3000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa w