Jeshi la Nigeria huwakimbia Boko Haram

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Sultan wa Sokoto aitwaye Muhammad Sa'ad Abubakar

Viongozi wa juu wa dini ya kiislam nchini Nigeria wameli shambulia jeshi nchi hiyo na pia kuwashutumu kuwa hukimbia mashambulio yanayofanywa na kundi la kigaidi la kiislam la Boko Haram.

Bodi hiyo inayoongozwa na Sultan wa Sokoto,imesema kwamba jeshi hilo limekuwa na tabia ya kutelekeza silaha zao kwa jeshi na kukimbialia mafichoni , na pindi mambo yanapotulia hurejea uraiani na kuwatishia raia.

Maelfu ya raia wa Nigeria wamekimbilia Niger kufuatia shambulio la hivi karibuni kutoka kwa kundi hilo la Boko Haram.

Waasi hao hujifanya kuwa ni wafanyabiashara walobebelea maboksi yenye bidhaa sokoni katika mji wa Damasak mji ulio Kaskazini mwa nchi ya Nigeria.

Lakini imebainika kwamba boksi hizo huwa zimesheheni bunduki,ambazo hutumika kushambulia raia wasio na hatia.