Rogders akubali lawama kipigo Liverpool

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema anapokea lawama zote kufuatia kipigo cha timu yake ya Liverpool ilichokipata kutoka kwa Cyristal Palace.

Liverpool ambayo msimu uliopita ilishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya England jana ilipata kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 3 -1 kutoka kwa Crystal Palace.

Rodger amesema amekubali kwamba ulikuwa ni wakati mgumu na analazimika kufanya juhudi kubwa ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo ndani ya Liverpool.

Amesema wamesikitishwa na kiwango cha timu pamoja na matokeo mabovu na kwamba kama meneja wa ni lazima achukue lawama.