Maharusi waoana ndani ya bwawa la maji

Haki miliki ya picha BBC World Service

Maharusi wawili walifanya harusi yao katika bwawa lenye lita milioni 1.5 za maji ya bahari .

Bwawa hilo hutumiwa kutoa mafunzo ya kupiga mbizi katika kituo cha Fort William.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bi Dorota Bankowska mpiga mbizi mzoefu aliolewa na mpenzi wake ambaye ni mwalimu James Abbot nyumbani kwao mjini Plock , Poland mwezi jana lakini akataka sana kufanya jambo la kipekee wanakoishi kama ishara ya kusherehekea harusi yao.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bi Abbott alipokea mafunzo ya upigaji mbizi katika kituo hicho kilicho katika ufuo wa bahari ya Loch Linnhe mnamo mwaka 2007 na kuwaomba wafanyakazi wa kituo hicho wamruhusu afanye harusi yake chini ya maji hayo.

Bwawa hilo, hutumiwa kutoa mafunzo kwa wapiga mbizi pamoja na kufanyia majaribio vifaa vipya. Picha hizi zimetolewa na kituo hicho.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Bi harusi alivalia gauni nyeupe huku bwana harusi akivalia sketi ambayo huvaliwa na waskochi ijulikanao kama 'Kilt'.

Maharusi hao waliungana na marafiki wao Ala Bankowska na Charlie Cran-Crombien chini ya maji hayo.

Wote wanne walivalia vifaa vya kupigia mbizi pamoja na mavazi yao ya harusi.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Takriban wageni 100 walitazama harusi hio wakiwa nje

Bi Abbott anafanya kazi katika kiwanda cha mafuta na gesi.