Muda wa mazungumzo na Iran waongezwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kuna wasiwasi mazungumzo yatakamilika bila mwafaka kuhusu mradi wa nuklia wa Iran

Muda wa mwisho wa kufikia mwafaka katika mazungumzo kati ya Iran na nchi sita tajiri zaidi duniani kuhusu mpoango wake wa nuklia umeongezwa hadi Juni mwaka ujao.

Hii ni baada ya mazunguzo yanayoendelea mjini Vienna kukosa kufioka mwafaka uliotarajiwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond kusema wamepiga hatua za kuridhisha ingawa ni vigumu kufika mwafaka katika muda uliotarajiwa.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa China Wang Yi amasema kuwa anaamini mwishowe muafaka utapatikana.

Lakini taarifa kwenye mtandao wake ilisema kwa idadi kubwa ya masuala kadha ya kitaalamu yanatakiwa kuzungumziwa kwa undani.

Wapatanishi wanasema kuwa kuna pengo kuhusu masuala ya kuiondolea vikwazo Iran ili nayo iweze kuachana na mipango ya urutubishaji madini ya Uranium.

Kubwa kwa yote hayo ni kwamba muda unayoyoma kwa viongozi wa dunia kufikia mwafaka na Iran kuondoa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kuhusiana na mradi wake wa Nuklia.

Huku kukiwa na tofauti kati ya mataifa, inaonekana mazungumzo yanayoendelea mjini Vienna duru za kidiplomasia zinasema kuwa yataakhirishwa hadi Disemba.

Iran inashauriana na nchi nyingine sita zenye ushawishi zaidi dunaini ambazo zilikuwa zimejipatia hadi mwishoni mwa leo kuwa na mwafaka.

Serikali ya Iran inasema kuwa inataka nishati ya nuklia kwa matumizi ya kawi ya atomiki wala sio kutengeza silaha za nuklia.

Marekani, Urusi, China na Ufaransa, pamoja na Ujerumani, zinajaribu kufikia mwafaka wa pamoja kuhusiana na mkataba uliofikiwa mjini Geneva mwaka jana.

Mazungumzo ya ngazi ya juu yanaendelea kati ya waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mawaziri wa mataifa mengine matano.

Katika miezi michache iliyopita, mazungumzo yamepunguza wasiwasi kuhusu vita vipya mashariki ya kati na mawaziri watakuwa na wasiwasi kuondoka Vienna bila ya kupata mwafaka.