Mama ashtakiwa kutupa mtoto Sydey

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtoto anayekisiwa kuwa na umri wa wiki moja aliokotwa na waendesha baiskeli

Mama mmoja nchini Australia anashtakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji dhidi ya mtoto wake mchanga ambaye alikutwa akilia katika eneo alilotelekezwa kwenye mfereji unaopitisha maji machafu pembeni ya barabara mjini Sydney,ambapo Polisi wanakisia kuwa mtoto huyo alikuwa katika eneo hilo kwa siku tano.

Waendesha baiskeli walisikia sauti ya mtoto ikitokea kwenye eneo hilo siku ya jumapili.

Mwanamke huyo,Saifale Nai alitiwa nguvuni na Polisi baada ya msako uliodumu kwa saa kadhaa kwa kupata taarifa katika hospitali na operesheni ya nyumba kwa nyumba.

Polisi inasema mtoto huyo wa kiume alitupwa tangu siku ya jumanne .

Taarifa za mahakama zinasema mwanamke huyo alikubali kuwa alimtupa mtoto wake katika mfereji huo akiamini kuwa angekufa.

Mtoto huyo anaelezwa kuwa yuko hospitalini na hali yake inaendelea vizuri.