Mfanyakazi mkatili matatani Uganda

Image caption Polisi wamemkamata Jolly Tumuhirwe aliyemtendea ukatili mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu

Polisi wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji.

Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wenegine.

Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso.

Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba.

Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka.

Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu.

Afisaa mkuu wa polisi Fred Enaga, amewaonya waajiri kuchunguza mbinu zinazotumika kuwachagua wasichana wa kazi, kwa sababu matendo kama haya yanaweza kutokana na matatizo ya kisaikologia.

Waziri wa Jinsia, Kazi na maendeleo ya jamii Bi Mary Karooro Okurut alipongeza juhudi za wazazi wa mtoto huyo Arnella "kutokana na kitendo hicho kwa mtoto. Ingekuwa mtu mwingine angemuua mischana huyo wa kazi lakini alifuata sheria. Pia tunapeleka marekebisho katika katiba kuhusu maslai ya watoto bungeni kuimarisha sheria zinazowajali watoto," alisema waziri huyo.

Polisi wamesema kuwa nia ya shambulio hilo haijatambulika na pia msichana huyo amefanyia kazi familia hiyo kwa siku 26 pekee. Wazazi wamesema kuwa mtoto huyo ametolewa hosipitalini na hali yake ya afya inaimarika.

Kulingana na msemaji wa polisi Fred Enaga, kesi hiyo iliripotiwa na Baba ya mtoto Erick Kamanzi mnamo tarehe 13 Novemba katika kituo cha polisi cha Kiwatule baada ya kuona video hio.

Kesi hiyo ilipelekwa kwa kitengo cha polisi cha Kiira. Baada ya uchunguzi, msichana huyo wa kazi alihukumiwa na shataka la mateso katika mahakama ya Nakawa na kuzuuliwa katika gereza la Luzira.

Bwana Enaga alisema Bi Tumuhirwe alishtakiwa chini ya kifungo cha tatu kwenye katika kinacholinda maslahi ya watoto. Kifungo hicho kinajumuisha mashataka kama ya kutesa inayopeana uwezekano wa kumfunga mtu hadi miaka 15 gerezani.

Hata hivyo, Bwana Enaga anashauriana na mkurugegenzi wa pande za mashtaka kurebisha hukumu hilo kuwa kifungu cha maisha.