Ripoti ya ufisadi kuwasilishwa bungeni

Image caption Wabunge wa Tanzania

Kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali, katika Bunge la Tanzania itawasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu sakata la ufisadi.

Uchunguzi huo ni kuhusiana na fedha zilizochotwa katika akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu ya nchi hiyo.

Dola zipatazo milioni 122 zinadaiwa kuchotwa isivyo halali katika akaunti ya pamoja kati ya kampuni ya kufua umeme ya IPTL na Shirika la Umeme Tanzania.

Tayari baadhi ya wahisani kutoka nje wameamua kusitisha misaada na mikopo kwa serikali ya nchi hiyo hadi hapo sakata la ufisadi huo litakapopatiwa ufumbuzi.