Mzee wa miaka 84 apotea majini Sydney

Image caption Picha ya Meli ya Sun Princess iliyopigwa mwaka 2009.inayoelezwa mzee wa miaka 84 alianguka

Maafisa nchini Australia wamesitisha zoezi la kumtafuta mzee mmoja mwenye umri wa miaka 84 ambaye alikisiwa kuwa alianguka baharini mashariki mwa mji wa Sydney.

Mtu huyo ambaye jina lake halikutajwa, alipotea majira ya usiku

Mamlaka ya usalama wa majini imesema hakuna dalili ya kuwepo kwa mwanaume huyo na si rahisi kuwa hai katika eneo analoelezwa kuangukia kutoka kwenye meli , umbali wa mita 25.

Meli ya kampuni ya Princess Cruises, ilisitisha safari yake kwa muda kuelekea Sydney wakati operesheni ya kumtafuta mzee huyo ilipokua ikifanyika.

Msemaji wa mamlaka ya usalama wa baharini(AMSA) Mal Larsen amesema mazingira ya tukio hilo bado hayafahamiki.

Mamlaka hiyo imesema picha za kamera ya CCTV zinaonyesha mwanaume huyo akianguka umbali wa mita 25 kutoka kwenye Meli,hata hivyo imeelezwa kuwa si rahisi kumpata akiwa hai.