Hali ya usalama Missouri yaimarishwa

Haki miliki ya picha NC
Image caption Jay Nixon Gavana wa Missouri

Gavana wa jimbo la Missouri nchini marekani ameomba nguvu zaidi za kijeshi kuelekezwa Ferguson kufuatia vurugu zilizotokea mapema wiki hii.

Gavana Jay Nixon amesema kwamba kikosi cha jeshi cha ziada cha taifa hilo watasaidia kulinda mali na uhai.lakini meya wa jiji la Ferguson ,James Knowles amekinza upelekwaji wa kikosi hicho za ziada na kuhoji kwanini wapelekwe sasa,kikosi hicho kinapelekwa kikiwa kimechelewa, na kuuita uamuzi huo kuwa ni usumbufu.

Meya huyo amedai kwamba vitendea kazi vyote vilivyopaswa kuandaliwa vilipaswa kuwa tayari kukinga uharibifu wa mali na kuepusha majeruhi, nyumba zaidi ya kumi na mbili zilichomwa moto askari wapatao mia saba wametawanywa katika maeneo tofauti yapatayo miamoja kuhakikisha usalama.