Deegbe aliacha kazi Benki na kujiajiri

Makala ya Ndoto ya Afrika inaeleza habari kuhusu Wajasiriamali wanane kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika kila mmoja akieleza changamoto alizozipata alipokua akianza.

Hivyo, katika mfululizo huu utapata fursa ya kujifunza katika kufikia ndoto, ndoto zao, na kama waliweza kuzisimamia.

Mbali na kutokua na elimu katika soko la viatu, Fred Deegbe, ambaye alikua mfanyakazi wa Benki,aliamua kubadili mwelekeo, aliungana na rafiki yake na kuanzisha kampuni yao iitwayo, Heel The World (HTW) Kampuni kubwa ya kutengeneza viatu yenye makazi yake, Accra Ghana, hiyo ilikua mwaka 2011, na mwaka mmoja baadae Deegbe aliacha kazi ya Benki na kuweka nguvu zake katika kazi yake hii mpya.

Image caption Mjasiriamali Deegbe,hutoa elimu kwa wengine ili kutimiza malengo yao

Mjasiriamali huyu mdogo anataka kututhibitishia kuwa viatu vyenye ubora vinaweza kutengenezwa nchini mwake.

Heel The World, ambayo ina waajiriwa saba wa kudumu, ina mtandao wake maalum kwa ajili ya shughuli zote za kutangaza soko na biashara yake hii inategemea mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa, katika shughuli za kutafuta masoko.

Ni jinsi gani unaweza kukuza biashara yako kushindana na Soko la bidhaa kutoka China?

Deegbe anasema: Bidhaa za China siku zote hazinitii hofu, na sababu kubwa, nimejiwekea kanuni mimi na ninaofanya nao kazi, niliweka kanuni hizo tangu mwanzo kuwa:

-Ushindani ni mzuri wakati wote lakini ni rahisi kumudu, hivyo ninahakikisha Kampuni yangu mara zote inatengeneza bidhaa nzuri ili ziweze kupendwa kwa namna tunavyotaka.

-Moja ya mikakati niliyonayo tangu awali ni kulenga soko linalofaa.

Image caption bidhaa kutoka Heel The World

-Nimetumia muda wangu na kuwekeza sana kwenye aina ya bidhaa na soko la bidhaa zangu.

-Tangu mwanzo wa Biashara yangu niliweka akilini kuwa bidhaa ya Kampuni yangu itakuwa ya kutengeneza kwa mkono kuliko mashine.

-Kuwafanya wateja kuwa marafiki. Hili ni suala muhimu sana, kupitia biashara hii, nasaidia pia viwanda vya hapa nyumbani.

Kwa sababu Watu hasa vijana wachache wana ajira na kuwa wanakosa elimu ya ujasiriamali tuna kitengo cha uwezeshaji kinachowasaidia Watu wanaotamani kuwa Wajasiriamali na wengine wanaotaka kuwa wajasiriamali wabunifu.

Tumeanzisha Semina tukishirikisha shule za sekondari, Vyuo vikuu pia Taasisi mbalimbali kama UT Bank.

Image caption Deegbe anasema bidhaa yake inakidhi viwango vya kimataifa

tunaajiri na kushirikiana na Watu wabunifu ambao tunaamini kuwa wanaweza kushidana kwenye Soko la Dunia.

Tumekua tukitoa mafunzo kwa Watu wanaotaka kujifunza kuhusu utengenezaji wa Viatu na kazi nyingine za ngozi, na kuwafundisha namna ya kupata wateja kwa mitindo ya aina mbalimbali ya bidhaa.

Kampeni ya kuwa washindi katika bidhaa zilizotengenezwa Ghana, Afrika:tunathamini bidhaa zetu wenyewe na tumekuwa tukizifanyia kampeni kwa miaka mingi kuwa hizi ni bidhaa za nyumbani.

Shanga zetu zimetengenezwa kwa vipande vya chupa na shaba nyeupe, vyupa hivyo vinatoka kwenye chupa xa Guinness ambazo hutupwa, na shaba kutoka kweye vyuma kutoka kwenye magari mabovu ya zamani.

Kulenga Soko:tunalenga Soko la bidhaa zetu kupitia mitandao ya kijamii pia kwa kuonana ana kwa ana na Wateja, ni biashara ambayo imekua kwa haraka na kwa mara zote tumetaka kuwapa Wateja wetu huduma bora na bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

Baada ya kulifikia Soko la nyumbani na kufanikiwa kwenye hilo, sasa tunadhamiria kupeleka bidhaa kwenye Soko la nje, na nimefanikiwa.Hatua hii inahitaji Ubora wa hali ya juu.