Hali ya raia wa Syria si ya kuridhisha

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Valerie Amos

Mkuu wa masuala misaada ya kibinadamu kutoka umoja wa mataifa ameeleza kuwa zaidi ya watu milioni kumi na mbili nchini Syria watahitaji misaada wakati wa majira ya baridi.

Akizungumza katika mkutano wa umoja wa mataifa juu ya usalama, Valerie Amos amesema kikosi cha misaada ya kibinadamu kutoka Uturuki na Jordan kimeleta tofauti katika maisha ya watu waliokuwa wamezongwa na mgogoro ingawa kikosi hicho hakijafanikiwa kuwafikia raia walio wengi kama yalivyokuwa matarajio yao.

Valerie amelitaka baraza la usalama kutoa ruhusa ya kufunguliwa mipaka ili kuruhusu misaada hiyo kuwafikia walengwa kabla haijakwisha muda wake wa matumizi unaokadiriwa kuwa mapema mwezi January.

Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon, ameishutumu serikali ya Syria na vikosi vya jeshi kwa kuendelea kulenga raia.