ZANU-PF kwafukuta

Image caption Joyce Mujuru matatani

Makamu wa raisi nchini Zimbabwe,Joyce Mujuru anapaswa kujiuzulu nyadhifa zake katika serikali na chama tawala cha ZANU-PF na hivyo kumuweka katika mazingira ya sintofahamu asijue majaaliwa ya harakati zake za kisiasa nchini humo.

Joyce anashutumiwa kufanya jaribio la mauaji ya Raisi Robert Mugabe mwenye umri wa miaka tisini madai ambayo yeye anayaona kwamba ni kashfa kwake.

Mke wa Rais,Grace Mugabe miezi ya karibuni amekuwa akiongoza kampeni dhidi ya makamu wa raisi huyo kwa madai kuwa Joyce anataka kumzidi kete mumewe.

Nayo mikutano ya hadhara aliyokuwa akiifanya makamu raisi huyo imeshindwa kutetea nafasi yake.