Maelfu ya dola kuikarabati Brisbane

Haki miliki ya picha WARREN DANIELS
Image caption Brisbane mvua yahanikiza

Mji wa Brisbane nchini Australia umekumbwa na dhoruba mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.mji huo ulipigwa na mawimbi makubwa na upepo mkali wenye nguvu ya kilomita mia moja na arobaini kwa saa.

Kimbunga hicho chenye nguvu nyingi kimeezua mapaa ya nyumba kadhaa,kuvunja madirisha,matofari yalionekana yakinyanyuliwa na kutupwa na kusababisha nyumba takriban elfu sabini kukosa nishati ,ni mwezi mmoja sasa mvua nyingi zinaendelea kunyesha kila siku kwa nusu saa na hivyo magari yanaonekana yakielea kwenye mitaa iliyofurika maji.

Jeshi nchini humo limeombwa kusaidia kusafisha miji ili kurejea katika hali yake ya kawaida,nayo serikali ya Queensland imekadiria gharama za ukarabati ulisababishwa na kimbunga hicho kwamba huenda ukagharimu mamilioni ya dola za kimarekani.