Duka lawakataa wateja wa kichina

Haki miliki ya picha BBC CHINESE
Image caption Maduka ya Uchina

Duka moja la nguo mjini Beijing China limezua mjadala nchini humo baada ya kuweka maelezo yanayopiwapiga marufuku wateja wake raia wa Uchina.

Duka hilo limehusishwa katika mgogoro wa ubaguzi wa rangi baada ya kuweka maelezo yanayosema ''Raia wa Uchina hawaruhusiwi ,isipokuwa wafanyikazi pekee kulingana na gazeti rasmi la Beijing.

Kulingana na mfanyikazi mmoja wa duka hilo,wateja wa kichina wanaudhi kwa kuwa wanawake wa kichina hujaribu nguo nyingi katika duka hilo bila kununua.

Duka hilo pia lililazimika kumlipa mteja wake mmoja raia wa kigeni dola 5,000 baada ya kipochi chake kuibwa huku ukanda wa video wa CCTV ukionyesha kuwa mtenja mmoja raia wa Uchina ndiye aliyemwibia.

Lakini mfanyikazi mwengine amesema kuwa lengo la duka hilo haswa ni kuwazuia washindani wake kuiga mtindo wa ngu za duka hilo.

Image caption Wateja wakiwa katika duka la Uchina

Maelezo hayo yamezua lalama katika mitandao ya kijamii huku mtumiaji mmoja wa mtandao wa Weibo akiuliza iwapo taifa hilo bado ni Uchina ama vipi.

''Duka la aina hii ni muhimu iwapo litafungwa'',alisema mtumiaji mwengine wa mtandao wa Weibo.

Mwengine aliandika ''kunifanyia maeonevu nyumbani kwangu'',alisema mtu mwingine huku akiongezea kuwa haoni kwa nini mmiliki wa duka hilo aliamua kulifungua nchini uchina iwapo hawataka wateja wa Uchina.

Lakini wataalam wa sheria wameliambia gazeti la vijana la kila siku mjini beijing kwamba huku maelezo hayo yakiwa ya kibaguzi,mmiliki wa duka hilo hajakiuka sheria kwa kuwa Uchina haina sheria ya kupinga ubaguzi wa rangi.