Mabomu yarindima Nigeria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Taharuki ya mabomu

Watu wapatao ishirini na watano wamekufa kufuatia shambulio la bomu katika jimbo la Adamawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Imetaarifiwa kwamba wote waliouawa katika shambulio hilo ni raia na watano askari.tukio hilo limetokea karibu na mji wa Mubi ambao mwezi huu ulikuwa ukishikiliwa na vikosi vya serikali ya nchi hiyo baada ya kuukomboa kutoka katika himaya ya wanamgambo wa kikundi cha kiislam cha Boko Haram.

Kuna matukio kadhaa ya mashambulizi yanayofanywa na kundi la Boko Haram katika siku za hivi karibuni ikiwemo na matukio mawili ya kujitoa muhanga kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri,shambulio ambalo liligharimu uhai wa watu nane.