Bunge Nigeria lataka Shell ilipe fidia

Image caption Shell ilipinga ripoti kuwa ilikuwa na ufahamu kuhusu mafuta kuvuja kutoka katika mabomba yake

Bunge nchini Nigeria limesema kampuni kubwa ya mafuta Shell inapaswa kulipa karibu dola bilioni 4 kama fidia kwa familia zilizoathirika na kuvuja kwa mafuta kutoka kwa mabomba yake mwaka 2011.

Shirika la serikali , ambalo lilichunguza tukio hilo lililohusu tanki moja ya mafuta katika machimbo ya mafuta ya Bonga , amesema mafuta hayo yaliyovuja eneo la mwambao yalienea eneo la karibu kilometa za mraba elfu moja .

Malipo ya fidia ya takriban dola bilioni 11 yalipendekezwa awali .

Uamuzi huo wa bunge si wa mwisho, kwa sababu lina mamlaka tu ya kupendekeza , na si kushurutisha utozaji wa faini .

Kampuni ya shell awali ilisema imesafisha mafuta yote yaliyovuja. Jimbo la Niger delta limechafuliwa kwa kiasi kikubwa na mafuta yanayovuja , mengi yakivuja kutokana na wizi wa mafuta na hila za upasuaji mitambo ya mafuta