Vijana 70 wahukumiwa vifungo Misri.

Haki miliki ya picha
Image caption Vijana katika mji wa Alexandria nchini Misri

Mahakama moja nchini Misri imewahukumu vifungo gerezani vijana 70, kwa kuhusika kupanga mkutano na kundi lililopigwa marufuku.

Mahakama hiyo iliyoko katika mji wa Alexandria imewahukumu vijana hao baada ya kuhusika katika mkutano uliopangwa na kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.

Televisheni ya taifa ya nchi hiyo imesema kuwa wavulana hao wenye umri kati ya miaka 13 na 17, awali waliziba barabara, kuwasha moto magurudumu na kisha kuharibu mali ya watu.