Afrika yawika katika orodha ya FIFA

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mataifa ya afrika yashamiri katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani FIFA

Guinea ndio taifa la Afrika ambalo limepanda juu zaidi katika orodha ya FIFA duniani mwezi wa Novemba.

Taifa hilo limepanda nafasi 17 katika orodha hiyo ya dunia hadi nafasi ya 38 huku wakipanda hadi katika nafasi ya 6 kutoka ya 11 barani afrika.

Kuimarika kwa Guinea kunatokana na ushindi wao dhidi ya Togo na Uganda ambo uliwasaidia kufusu katika kombe la Afrika mwaka 2015.

Mali ambayo pia ilifuzu katika michuano hiyo ya Afrika ilipanda nafasi tisa zaidi hadi nafasi ya 49 duniani na kuorodheshwa ya 10 barani Afrika.

Hatahivyo Misri ilipoteza nafasi 22 na hivyobasi kushuka hadi nafasi ya 60 duniani na 14 barani Afrika.

Kwa jumla matokeo hayo yalikuwa mazuri kwa soka ya Afrika,huku mataifa 10 kutoka bara hili yakiorodheshwa katika nafasi hamsini bora duniani.

Mataifa 10 bora ya Afrika katika orodha ya FIFA duniani.

1. Algeria (18)

2. Tunisia (22)

3. Ivory Coast (24)

4. Senegal (35)

5. Ghana (37)

6. Guinea (38)

7. Cape Verde (39)

8. Cameroon (41)

8. Senegal (41)

9. Nigeria (42)

10. Mali (49)