Mahakama kuamua kuhusu kesi ya Mubarak

Image caption Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak akisikiliza kesi yake.Mahakama inatarajiwa kuamua kuhusu kesi hiyo

Mahakama nchini Misri inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kesi inayomkabili rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak kufuatia mashtaka ya mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa mandamano ya mwaka 2011.

Bwana Mubarak alipatikana na makosa hayo miaka miwili iliyopita lakini mahakama ya rufaa ikabatilisha uamuzi uliotolewa wa kifungo cha maisha gerezani.

Uamuzi wa kesi hiyo ulitarajiwa kutolea mwezi Septemba lakini jaji alisema kuwa alitaka muda zaidi kuchunguza ushahidi ulio na kurasa 160,000.

Hata kama Mubarak hatapatikana na hatia hataachiliwa kwa kuwa tayari anatumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kufuja pesa za umma.