WHO:Watu 7000 wamefariki na ebola

Haki miliki ya picha EPA
Image caption WHO imesema kuwa takriban raia 7000 wamefariki na ebola kufikia sasa

Hesabu mpya kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO inaonyesha kuwa karibu watu 7000 wameaga duian kutokana na ugonjwa wa Ebola wengi wakiwa eneo la Afrika magharibi.

Hili ni ongezeko la zaidi ya watu 1000 tangu WHO itoe hesabu yake ya mwisho siku nne zilizopita.

Sehemu kubwa ya ongezeko hilo iliripotiwa nchini Liberia

Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa unaohusika na ugonjwa wa Ebola Antony Banburry anasema kuwa kwa sasa nchi iliyoathirika zaid ni Sierra Leone ambapo karibu visa 500 vya ugonjwa wa Ebola huripotiwa kila wiki.

Amesema kuwa maziko ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha maambukizi bado hayafanywi kwa njia iliyo salama.