Wasichana shupavu washinda wanaume

Msichana wa India Haki miliki ya picha Getty

Video inayoonesha wasichana wawili wanafunzi wakipigana na vijana kwenye basi katika jimbo la Haryana kaskazini mwa India, imekuwa habari kubwa huko.

Wasichana hao wawili ambao ni ndugu, wanasema walisumbuliwa na vijana na walipolalamika walishambuliwa.

Katika mitandao ya jamii wasichana hao wanasifiwa na wamepewa jina la "shupavu wenye moyo" kwa kupigana kwa hamasa.

Wengine wanauliza kwanini abiria wengine hawakuingilia kati.

Wasichana kusumbuliwa hadharani limekuwa swala kubwa nchini India baada ya msichana kubakwa na hatimaye kufa kwenye basi mjini Delhi karibu miaka miwili iliyopita.