Polisi,waandamanaji wapambana Hong Kong

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Waandamanaji Hong Kong

Polisi na waandamanaji wanaodai demokrasia wamepambana mjini Hong Kong katika eneo linalozunguka makao makuu ya serikali.

Ili kutuliza maandamano hayo Polisi wamelazimika kutumia maji yenye pilipili ambao baadhi yao walikuwa wamejihami kwa silaha.

Takribani watu 48 wanashikiliwa na polisi kutokana na maandamano hayo ambayo yamechukua miezi miwili hadi sasa.

Madai ya waandamanaji hao ni kutaka kuwa na uhuru wa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na Beijing.