Mashine yenye uwezo wa kufikiri kitisho

Image caption Prof Stephen Hawking

Profesa Stephen Hawking, mmoja wa wanasayansi mahiri nchini Uingereza, amesema juhudi za kutengeneza mashine inayofikiria inatishia uwepo wa binadamu.

Ameiambia BBC:"Kutengenezwa kwa mashine yenye uwezo wa kufikiria inaashiria maangamizi ya binadamu."

Onyo la Profesa Hawking limekuja kutokana na kuimarishwa kwa teknolojia anayotumia katika mawasiliano, ambayo inahusisha msingi wa Akili Bandia(Artificial Intelligence, AI).

Lakini wengine hawana upinzani sana na matarajio ya teknolojia hiyo ya AI.

Mwanasayansi huyo wa nadharia ya fizikia, ambaye anaumwa ugonjwa wa mishipa ya fahamu (ALS), anatumia mfumo mpya uliotengenezwa na kampuni ya Intel kuzungumza.

Image caption Wanasayansi wakifuatilia kifaa chenye muundo wa kufikiri kama binadamu

Wataalam wa mashine za kujifunza kutoka kampuni ya Uingereza ya Swiftkey pia walihusika katika kunda mashine hiyo. Teknolojia yao, tayari inatumika kama mfumo wa smartphone, unajifunza namna profesa Hawking anavyofikiria na kupendekeza maneno ambayo huenda angetaka kuyatumia baadaye.

Profesa Hawking amesema miundo duni ya akili bandia (AI) ambayo imeboreshwa mpaka sasa imethibitisha kuwa na manufaa sana, lakini ana wasiwasi wa madhara yanayotokana na kuunda kitu chenye uwezo sawa na binadamu au kupita. "Mashine hiyo inaweza kujiwasha na kujizima na kujibadili yenyewe katika kiwango kisichomithilika," amesema.

Cleverbot ni kifaa(software) ambacho kimeundwa kuwasiliana kama binadamu anavyofanya "binadamu ambao wana ukomo wa kufikiri kutokana na mabadiliko ya taratibu ya kibaolojia, hawawezi kushindana na mashine hii, na watapitwa kwa mbali."