Instagram yamtia matatani Balotelli

Image caption Mario Balotelli

Shirikisho la soka FA linachunguza ujumbe wa Instagram wa mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli unaodaiwa kuwa ni wa kibaguzi.

Ballotel mwenye umri wa miaka 24 akijibu shutma dhidi yake kutokana na ujumbe wake mtandaoni aliandika tena ujumbe usemao “mama yangu ni Myahudi wote nyamazeni kimya”.

Hata hivyo Balotelli anadaiwa kuufuta haraka haraka ujumbe wa awali aliouandika ambao unadaiwa kuwa ni wakibaguzi.

Msemaji wa Liverpool anayochezea Balotell amesema kuwa wanataarifa kuhusiana na ujumbe huo na kwamba watafanya mazungumzo na Balotell.

Shirikisho la soka FA limesema kuwa linataarifa kuhusiana na mchezaji huyo kuiweka taarifa hiyo katika Instagram na kisha kuifuta baadae.

Mkurugwenzi wa zamani wa shirikisho la soka Simon Johnson anasema Balotell anastahili kuchukuliwa adhabu kwa kitendo hicho