Mitandao ya Sony yaingiliwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Askari wa Korea Kaskazini

Kampuni ya picha ya Sony kutoka nchini Marekani inachunguza hujuma ya mitambo yake kimitandao kutofanya kazi sawa sawa kutokana na madai ya kuhujumiwa kwa mfumo kwa mitandao yao.

Matokeo ya kutofanya kazi vilivyo kwa mitambo hiyo kumesababisha kushindikana uchapishaji picha za kimitandao.

Hata hivyo kuna uvumi kwamba huenda Korea Kaskazini wanahusika na hujuma hiyo ya kimitandao dhidi ya kampuni ya Sony.

Kuhusishwa kwa Korea Kaskazini katika hujuma hiyo ni kufuatia madai ya kampuni hiyo kutaka kutoa kazi yake mpya inayoonyesha harakati za CIA kutaka kumuua kiongozi wa Pyongyang.

Shirika la upelelezi la Marekani FBI limethibitisha kwamba linachunguza ukweli wa uvumi huo kuhusisna na hujuma za kimitandao dhidi ya kampuni.