Zaidi ya miaka 30, ukimwi bado tishio

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya miaka 30, madhara ya ukimwi bado yanaonekana Tanzania, kijamii na kiuchumi

Zaidi ya miaka 30 tangu mgonjwa wa kwanza wa ukimwi kugunduliwa Tanzania, lakini madhara yake bado yanaonekana: kiuchumi na jamii.

Mwandishi wa BBC Halima Nyanza alitembelea eneo la Rukunyu wilaya ya Rakai nchini Uganda kilomita chache tu kutoka mpaka wa Tanzania, panapoelezwa kuwa chanzo cha ugonjwa huo kuingia Tanzania kupitia wafanyabiashara.

Kijiji cha Nyangoma kilichopo eneo la Rukunyu katika miaka ya 80, kilikuwa chachu ya maendeleo katika eneo la nchi za Afrika mashariki, kutokana na Gulio kubwa lililowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi tano za eneo hilo.

Takriban miaka 30, kwa ugonjwa hatari wa ukimwi, kuua wafanyabiashara wengi, waliokuwa wakikutana katika eneo hilo, wakazi wa eneo hilo wanasema hali ni mbaya kiuchumi na kijamii. Umasikini na ugonjwa wa ukimwi bado unaendelea taratibu kumaliza watu.

Eneo hilo la Rukunyu, ndipo linaelezwa kuwa ndio chimbuko la wafanyabiashara wa mwanzo wa Kitanzania waliokufa na ugonjwa wa ukimwi. Na hatimae ugonjwa huo ukasambaa katika maeneo ya Kanyigo mkoani Kagera Tanzania na hatimaye Tanzania nzima.