Iran yajitegemea katika vita dhidi ya IS

Image caption Ndege za kijeshi za Marekani

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema inaamini Iran imefanya mashambulio ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika maeneo ya mashariki mwa Iraq.

Ndege za kijeshi za Iran za F4 zimeripotiwa kuyashambulia maeneo ya IS katika jimbo la Diyala nchini Iraq.

Marekani pia inaendesha mashambulio ya anga katika eneo hilo, lakini msemaji wa Pentagon, Rear Admiral John Kirby, amesisitiza kuwa Marekani haishirikiani na Iran katika vita dhidi ya Islamic State. Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi wa Iran pia ametupilia mbali kuwepo kwa mazungumzo yoyote ya ushirikiano na Marekani.