Wakimbizi ni kama mateka Australia

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Waziri wa Uhamiaji wa Australia Scott Morrison

Chama cha upinzani nchini Australia kimeilaumu Serikali ya nchi hiyo kwa madai inawatumia wakimbizi kinyume na sheria kwa maslahi ya kisiasa.

Mawaziri nchini humo wanalishinikiza baraza la seneti kubadili sheria dhidi ya wakimbizi ili waweze kuwatumia kama mateka wa kisiasa.

Waziri wa uhamiaji Scott Morrison amewasilisha hoja kadhaa ili kushawishi upitishwaji wa muswada unaolenga kuwa na sheria mpya dhidi ya waomba hifadhi na wakimbizi..

Hata hivyo kiongozi mkuu wa upinzani Tony Burke amesema serikali yao imekuwa ikikaa na wakimbizi hao kama wahalifu kinyume na sheria za kimataifa za haki kwa wakimbizi.

Australia kwa sasa inaihifadhi idadi kubwa ya waomba hifadhi na wakimbizi wanaoingia nchini humo kwa njia ya boti na kuwapeleka kambi za Papua na New Guinea na Nauru.