Familia ya mateka yasihi Al Qaeda kumwachilia

Haki miliki ya picha
Image caption Familia ya Like Somers

Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen.

Rais Barack Obama aliidhinisha kikosi cha kumwokoa Luke, mwezi uliopita.

"Kwa masikito, Luke hakuwepo, japokuwa mateka kutoka mataifa mengine walikuwepo na waliokolewa," Baraza la Usalama la Taifa, limesema.

Mtu anayejitambulisha kama Luke Somers, ambaye alitekwa mwaka 2013, ameonekana katika video, akisema maisha yake yako hatarini na anaomba msaada.

Video hiyo pia inamwonyesha mfuasi wa al-Qaeda huko Yemen akitishia kumuua Bwana Somers hadi madai yao ambayo hayajatajwa, yatakapotimizwa.

Bwana Somers, mwenye umri wa miaka 33, alifanyakazi kama mwandishi wa habari na mpiga picha wa mashirika ya huko na kazi zake zikaonekana katika vyombo vya habari vya kimataifa, ukiwemo mtandao wa BBC.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Luke Somers raia wa Marekani mwandishi wa habari anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda huko Yemen

Familia ya Somers imetoa ombi kwa Al-Qaeeda kuwa na huruma na Somers na kumwachilia.

Mamake Somers alinukuliwa akisema: '' Tafadhali............tupeni nafasi kumuona Luke kwa mara nyingine.''

Katika kanda iliyowekwa kwenye mtandoa wa You Tube, mamake Somers pamoja na kakake, wamesema Luke alikuwa tu anajaribu kuwatendea mema watu wa Yemen. ''

"Luke ni mpiga picha tu na hana hatia ya kufanya chochote kibaya wala kwa vitendo vinvyofanywa na serikali ya Marekani, '' alisema kakake Somers.

Mwandishi huyo wa habari alikamatwa mwaka 2013 mwezi Septemba.

Somers, 3mwenye umri wa miaka 33, alifanya kazi kama mpiga picha na mwandishi na taarifa zake zilitumiwa na mashirika ya kimataifa yua habari ikiwemo BBC.