Dawa Michezoni zamchefua,Jenny Meadows

Haki miliki ya picha PA
Image caption Jenny Meadows

Mwanariadha wa Uingereza Jenny Meadows ana hofu kwamba itakuwa kashfa kubwa kuliko zote na ya wakati wote" iwapo tuhuma za kuenea na kufanyika udanganyifu michezoni miongoni mwa wanariadha wa Urusi zitakuwa kweli.

Meadows, alishindwa na mwanariadha wa Urusi kupata medali ya dhahabu katika michezo ya Ulaya mwaka 2011, amesema madai hayo "yanamnyong'onyeza".

Nyota huyo wa mbio za mita 800 pia amesisitiza michezo ya riadha haitakomesha kamwe matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 33 kutoka Wigan ameiambia BBC Sport: "Sifikirii kamwe kuwa ni vita tunavyoweza kushinda."

Makala ya kipindi cha televisheni ya Ujerumani, kilichotangazwa Jumatano, kimedai kuwaslisha ushahidi wa matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezo zikitumika kwa mpangilio na kuwepo Rushwa katika sekta ya michezo nchini Urusi.

Hata hivyo rais wa Shirikisho la Riadha nchini Urusi amekanusha madai hayo na kuyaita"uongo mtupu"