Mandela akumbukwa Afrika Kusini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kumbukumbu za Mandela

Raia Nchini Afrika Kusini wanaadhimisha mwaka mmoja tangu alipofariki Rais wa Kwanza mwafrika wa Afrika hayati Kusini Nelson.

Miongoni mwa yatakayojiri katika sherehe hizo ni pamoja na ibada ya maombi, sherehe za kuweka shada za maua na wakongwe waliopigana na makaburu na utawala wa ubaguzi wa rangi, na hatimaye mechi ya mchezo wa kriketi.

Kutakuwa na sherehe za upulizaji wa vuvuzela kote nchini humo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Hayati Mandela na aliyekuwa mkewe Graca Machel

Leo ni mwaka mmoja kamili tangu Mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini kufariki dunia.

Madiba alifariki usiku wa kuamkia Disemba tano mwaka uliopita akiwa na umri wa miaka 95.

Alikuwa Rais wa kwanza mzalendo kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka mitano kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipoachia madaraka kwa hiari yake.

Baadhi ya watu waloongea na BBC, ni mjukuu wa Mandela Ndileka Mandela.

Raia wa nchi hio wamebuni njia zao wenyewe za kumkumbuka Mandela aliyeongoza nchi hio kutoka kwa mikono ya wabeberu.Alifungwa miaka 27 jela.

Maduka mengi ya kuchora Tatoo nchini humo yameripoti ongezekao la watu wanaochorwa picha ya Mandela au Tatoo za Mandela katika sehemu zao za mwili.