Watu 7 wafariki katika milipuko Somalia

Haki miliki ya picha AP
Image caption Milipuko iliotokea katika mji wa Baido nchini Somali.

Takriban watu saba wamefariki katika milipuko miwili ya kujitolea muhanga katika mji wa Baidoa kusini mwa Somali.

Shambulizi hilo ambalo pia liliwajeruhiwa zaidi ya watu 20 lilitokea nje ya mgahawa unaopendwa sana na wakaazi na wanahabari.

Wawili ya waliofariki ni waandishi wa habari wanaofanya kazi na runinga za Somali kulingana na BBC Somali.

Makundi kadhaa ya wanamgambo yamekuwa yakipigania udhibiti wa Somali tangu rais Siad Barre ang'atuliwe Mamlakani mwaka 1991.

Nahodha Hassan Nor ameliambia shiriki la habari la AP kwamba mlipuaji wa kujitolea muhanga aliliendesha gari lake katikati ya kundi la watu na kujilipua.

Mlipuko wa pili ulitokea baada ya mlipuaji mwengine wa kujitolea muhanga kujilipua ndani ya mgahawa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Milipuko somali.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Baidoa ,daktari Laahi Maxamed Aadan ameiambia BBC kuwa alipokea watu 41 mwendo wa saa kumi na mbili wengine wakiwa wametolewa baada ya kutibiwa majeraha madogo madogo.

''Watu saba tayari walikuwa wamefariki wakati wa shambulizi hilo.

Tuna habari kwamba zaidi ya watu saba walifariki katika milipuko hiyo miwili .

Lakini hospitali ilipokea watu saba pekee ambao walikuwa wameaga dunia''alisema.

Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulizi hilo.