Kimbunga chaangusha miti Ufilipino

Image caption Kimbuga hagupit chaangusha miti na kusababisha mvua kuwa Ufilipino

Kimbunga Hagupit kinaeleka eneo la kaskazini Magharibi mwa ufilipino kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa.

Zaidi ya watu 500,000 wamehama maeneo ya nyanda za chini lakini katika maeneo ya mashariki ambapo ndipo kimbunga hicho kilianza kupiga watu wameanza kurejea.

Kimbunga hicho kimeangusha miti na nyaya za umeme na pia kusababisha mvua kubwa

Hata hivyo kimbunga hicho hakijakua kikubwa jinsi ilivyotarajiwa kama kimbunga Haiyan cha mwaka uliopita kilichosababisha uharibifu mkubwa.