Japan katika kipindi cha mpito kiuchumi

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wafanyakazi wa Japan katika kiwanda cha kutengeneza vipuri

Takwimu za hivi karibuni kutoka katika serikali ya Japan zinaonesha kwamba uchumi wa nchi hiyo unashuka kwa asilimia 1.9 kwa mwaka.

Takwimu hizo,zinaanzia katika kipindi cha mwezi July hadi kufikia mwezi Septemba,na kuelezwa kuwa ni mbaya kulinganisha na ilivyokadiriwa na kusemwa wazi kuwa sasa Japan iko kwenye kipindi cha mpito.

Ushukaji huo wa uchumi unaelezwa kukumbwa kutokana na kupanda kwa kiwango cha ushuru wa kodi uliolenga kupunguza madeni ya umma.

Wakosoaji wa masuala ya uchumi wanasema kwamba kodi hiyo inawabana wateja katika manunuzi.kutokana na hali hiyo inakadiriwa kiwango kipya cha kodi kitapanda mwezi October,mwakani ingawa kwa sasa kimechelewa kwa miezi kumi na nane.