Wanajeshi kuongezwa kupambana na ISIL

Haki miliki ya picha video
Image caption Wanamgambo wa Islamic State, wanaolengwa kushambuliwa.

Muungano wa majeshi yanayopambana dhidi ya Islamic State yakiongozwa na Marekani, yako tayari kupeleka vikosi zaidi nchini Iraq.

Kamanda wa muungano wa majeshi hayo, Jenerali James Terry kutoka Marekani amesema kiasi cha wanajeshi elfu moja na mia tano wataanza kupelekwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanajeshi ya Iraq, wanaopambana na wanamgambo wa kiislamu.

Idadi ya washauri hao wa kijeshi itaongezwa kati ya wanajeshi wa Marekani zaidi ya elfu tatu, ambao Rais Obama tayari amewaidhinisha kupelekwa Iraq.

Bado haijawekwa wazi wanajeshi wengine wa ziada watatoka katika mataifa yapi.