Ajikimu kwa kuuza maziwa ya mama

Image caption Maziwa ya mama yanasemekana kuwa na madini ya kusaidia mwili

Rebecca Hudson, kutoka mjini Manchester,Uingereza amepata zaidi ya pauni 3,000 kwa kuuza maziwa ya mama.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 26, anasema kuwa wakati mwanawe alipozaliwa mapema mno , wiki kumi kabla ya siku iliyotarajiwa, matiti yake yakawa hayawezi kutoa maziwa.

Lakini baadaye alianza kupata maziwa mengi sana kupita kiasi.

Na kwa sababu mtoto wake alizaliwa kabla ya siku yake, alihitaji tu kutoa maziwa kidogo kama chakula cha mtoto wake aliyekua katika mashine hospitalini.

Alisema ''sikutaka kuyamwaga maziwa yaliyosalaa, kwa sababu ni kazi ngumu sana kwa mama kutoa maziwa kwenye Matiti yake.''

"kwa hivyo nilitafakari ili niweze kupata pesa za ziada, sioni ubaya wowote ikiwa nitayauza maziwa yangu. ''

Image caption Maziwa ya mama aliyohifadhiwa kwenye jokofu

Kwa hivyo Rebecca alikwenda kwenye mtandao wa Internet, na kugundua kuwa nchini Marekani kuna wanawake ambao tayari wanauza maziwa hayo. Hapo ndipo aliamua kuanza kuuza maziwa yake kwenye mtandao.

Ana wateja ambao yeye huwauzia maziwa yake kwa pauni 12.50 kwa kila chupa.

Wateja wake wengi huwa ni wanyanyuaji uzani ambao hutumia maziwa hayo yanayosemekana kuwa na madini muhimu sana kwa mwili, pamoja na wapishi ambao hutumia maziwa hayo kwa upishi. Kadhalika watu hununua maziwa hayo wakiamini kuwa inawapa nguvu za kimwili na kuwaezesha kingono.

Rebecca Hudson alisema kuwa kwake yeye kile ambacho wateja wake wanatumia kufanyia maziwa ni shauri yao, ''sitabagua na kuwauzia watu fulani na kuwaacha wengine.''

Alisema marafiki wake walimshangaa sana hasa kwa pesa alizoweza kupata kwa kuuza maziwa yake wakisema ni njia rahisi sana kujipatia pesa na kwamba wanatafakari kufanya hivyo na wao