Yaya aliyemtesa mtoto UG aomba msamaha

Image caption Jolly Tumuhirwe

Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajulia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.

Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.

Haki miliki ya picha
Image caption Jolly Tumuhirwe ameomba mahakama kumsamehe kwa kumtesa mtoto

Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.

Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.

Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mianne au adhabu zote mbili.