Haki itatendeka kwa wanafunzi:43 Mexico

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Baba wa Alexanda Mora akiwa na majonzi.

Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Mexico, Jesus Murillo Karam,ametoa ahadi kuwa hakutakuwa na uonevu wowote katika kesi ya kupotea kwa wanafunzi nchi humo miezi miwili iliyopita.

Kutoweka kwa wanafunzi hao kumesababisha maandamano ya wiki kadhaa nchini humo waandamanaji wakipinda rushwa na ukatili uliozunguuka kesi hiyo.

Bwana Karam amesema kwamba uchunguzi wa kusaka walikopotelea wanafunzi hao unaendelea mpaka hapo wahusika wa tukio hilo watakapokamatwa.

Zaidi ya hayo amethibitisha mwili wa mmoja kati ya wanafunzi hao arobaini na tatu kuwa umetambuliwa kuwa ni wa Alexander Mora,mwili uliogunduliwa katika jaa la taka katika jimbo la Guerrero.

Mwanasheria mkuu huyo wachunguzi mahiri wa miili kutoka nchini Austria wakiunganisha mifupa kwa kuifananisha na kipimo cha vinasaba vya ndugu wa marehemu huyo9,ndipo walipoutambua.