Watoto wa kiume Culcutta sio dili

Image caption Wanawake makahaba wa India

Polisi Mashariki mwa mji wa Calcutta nchini India, wanachunguza tukio la mwanamke ambaye jamii yake ilimtelekeza katika bwawa,kwa kushindwa kuzaa mtoto wa kike ambaye baadaye walimtegemea kuwa kahaba.

Mwanamke huyo aliokolewa na chama cha kujitolea kuwahudumia makahaba kabla hajalazimika kujitosa kwenye ukahaba kamili.

Mwanamke huyo aliiambia BBC kwamba familia ya wakwe zake walianza kumdhihaki baada ya kuzaa watoto wa kiume watatu mfululizo, na kufahamishwa kwamba familia hiyo kwa kawaida huwapeleka watoto wa kike wa ukoo wao kufanya kazi ya ukahaba, iweje yeye azae watoto wakiume watupu?