Obama atahadharisha vijana kuhusu Ubaguzi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Barack Obama wakati akitoa hotuba yake kuwaasa vijana wa Marekani kutofanya fujo

Rais Obama amewaomba vijana wawe wakakamavu katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi lakini pia wavumilivu kwani mageuzi hayapatikani kwa urahisi.

Kauli yake inajiri wakati maandamano yakiendelea Washington, New York na Berkeley dhidi ya uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama kutomshtaki maafisa wa polisi wazungu waliohusishwa na vifo vya wanaume wenye asili ya Kiafrika.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji mikubwa kulalamika ubaguzi wa rangi nchini humo

Katika mahojiano kwenye televisheni rais Obama amesema maandamano ni muhimu kukumbusha jamii kwamba maguezi bado hayajafanyika.

Lakini ameongeza kwamba maandamano hayo hayana maana iwapo yatakumbwana ghasia.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Prince William na mkewe Kate Middleton

Zaidi ya watu 200 wamekuwa wakiandamana katika miji mbali mbali hasa mjini New York wakilalamika kwamba polisi wanawalenga wamarekani weusi baada ya visa kadhaa vya vijana wamarekani weusi kuuawa katika siku za hivi karibuni.

Hayo yakijiri, mwanamfalme Prince William na mkewe Kate Middleton walihudhuria mechi ya mpira wa vikapu huku watu wakifanya maandamano kupinga vitendo vya polisi kuwaua watu mjini New York.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jay-Z na Beyonce wakielekea kuwaamkua prince William na mkewe Kate

Wawili hao walikutana na mchezaji mahiri LeBron James na wanamuziki Jay-Z na mkewe Beyonce katika uwanja wa Barclays Center, ambako Cleveland Cavaliers walimenyana na Brooklyn Nets.

Ulikuwa usiku wa sita kwa maandamano kuendelea nchini Marekani kufuatia uamuzi wa mahakama aDisemba tarahe tatu kutomfungulia mashitaka sifa mmoja aliyedaiwa kumuua mmarekani mweusi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jay Z na Beyonce wakiwaamkua Kate na mumewe Prince William

Prince William na mkewe,walionekana kwenye skiri kubwa ndani ya uwanja huo huku mashabiki wakiwashangilia.

Awali Prince William alikutana na Rais Barack Obama katika Ikulu ya White House na kutoa hutuba kwa maafisa wa Benki ya dunia kuhusu uhalifu unaotendwa dhidi ya wanyamapori.

Walitembelea makao ya kuwatunza watoto mjini New York.